Ijumaa 10 Oktoba 2025 - 18:58
Ustahimilivu na kujitolea Wapalestina kumeidhihirisha sura halisi ya Wazayuni

Hawzah/ Hujjatul-Islam Sayyid Nazir Abbas Taqavi katika hotuba yake amesema: “Muqawama wa Kiislamu, kwa kusimama kidete na kustahimili, umeishinda serikali ya Kizayuni katika nyanja za kijeshi na kisiasa, na umeufunua uso wake wa kweli mbele ya mataifa ya ulimwengu.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa pili wa “Siku ya Tufani ya Al-Aqsa”, maandamano makubwa yaliandaliwa kwa juhudi za Harakati ya Kuuamsha Umma wa Mustafa wa Pakistan katika jiji la Karachi.
Katika hafla hiyo, kundi la wanazuoni mashuhuri, wanaharakati wa kisiasa na kitamaduni, pamoja na watu kutoka tabaka mbalimbali walishiriki. Wasemaji walisisitiza nafasi muhimu ya muqawama wa Kiislamu na wakasifu uthabiti wa taifa la Palestina katika kusimama kwake dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Katika mkutano huo, Hujjatul-Islam Sayyid Nazir Abbas Taqavi, mwanachama mwandamizi wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika hotuba yake akirejelea matukio ya miaka miwili iliyopita, alisema:
“Miaka miwili ya muqawama imeonyesha wazi kwamba harakati za Kiislamu kama Hamas, Hizbullah, na Ansarullah, si tu kwamba zimeweza kumpiga adui wa Kizayuni katika uwanja wa vita, bali pia zimemshinda vibaya katika nyanja za kisiasa na kiitikadi. Vita ambavyo utawala wa Kizayuni ulidhani vingemalizika kwa siku chache, kwa hekima, uvumilivu na uimara wa wapiganaji wa muqawama, vimegeuka kuwa pambano refu na la kihistoria. Uendelevu huo ndio uliofanya sura ya kweli ya uhalifu wa Israeli ifahamike duniani kote, na mawimbi ya chuki dhidi ya utawala huu yakazagaa ulimwenguni.”

Wasemaji wengine katika hafla hiyo pia waliongeza kusema kuwa: “Israeli leo haina tena nguvu za kijeshi kama zamani, wala haijabakiwa na uhalali wa kisiasa. Marekani inajaribu kuficha kushindwa kwa utawala huu nyuma ya pazia la ‘mipango ya amani,’ huku ikijitahidi kuyatumia baadhi ya mataifa ya eneo hili kama vile Uturuki, Qatar, Saudia, na hata Pakistan kama nyenzo za kuishinikiza harakati ya muqawama wa Palestina. Lakini ukweli ni kwamba mipango hiyo yote ipo tu kwa manufaa ya Israeli na washirika wake, na haina faida wala fursa yoyote kwa taifa la Palestina.”

Sehemu nyingine ya hafla hiyo ilisisitiza kuwa: “Utawala wa Kizayuni leo umechoka kijeshi, umedhoofika kiuchumi, na kimaadili umegeuka kuwa chukizo kubwa miongoni mwa mataifa yote duniani.”

Wasemaji wengine walieleza: “Marekani na washirika wake, ambao wameshindwa katika uwanja wa vita, sasa wanajaribu kufikia malengo yao kwa hila na usaliti. Lakini historia imethibitisha kuwa dhulma haidumu, na usaliti mwishowe huharibu mataifa.”

Mwisho wa hafla hiyo, washiriki walisema wazi kwamba: “Harakati ya Mapambano ya Kiislamu leo ni yenye nguvu zaidi kuliko wakati wowote uliopita, na kwa kujitolea, imechora wazi mpaka baina ya haki na batili. Sauti ya muqawama sasa imekuwa ikiakisi dhamiri hai kwa mataifa huru duniani, ikiwaita wote waungane katika kuwaunga mkono watu wa Palestina.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha